The House of Favourite Newspapers

Lucy Anayedaiwa Kuuawa Kikatili Na Mpenzi Wake Azikwa Kimara, Dar (Picha +Video)

Simanzi, huzuni na vilio vimetawala kwenye maziko ya mrembo Lucy Haule ambaye anadaiwa kuwa ameuawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali kwenye moyo na mwanume aliyekuwa na uhusiano naye wa kimapenzi yaani boyfriend wake.

Maziko hayo yamefanyika hii leo Julai 27, 2024 katika Makaburi ya Mwandwanga – Kimara Temboni jijini Dar ambako ndiko lilipotokea tukio hilo baya katikati ya wiki hii yaani Jumatano iliyopita.

Kwa mujibu wa mama mzazi wa Lucy aliyezungumza na GLOBAL TV, siku hiyo ya tukio mwanaume huyo alifika nyumbani kwake na kumuomba aende kuwaona wazazi wake watambuane ili taratibu za ndoa zifuate.
Mama huyo amesema hakujua kama ndiyo ilikuwa siku ya mwisho kwa mtoto wake, kwani alimwambia kuwa yeye kama mzazi wa kike hawezi kwenda kwa wazazi wa mwanaume bali inabidi wao ndiyo waje na alivyomwambia hivyo akaondoka na ndiyo umekuwa mwisho wa Maisha ya binti yake Lucy.