Lugola Aagiza Nabii Eliya Mahela Akamatwe – Video

WAZIRI wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola, ametua katika kanisa Pentecostal Power Ministry na kuamuru kukamatwa kwa mchungaji wa kanisa hilo, Nabii Eliya Mahela, kwa kosa la kuendesha kanisa bila kusajiliwa na kusababisha kelele kwa wananchi walio jirani na kanisa hilo.

 

Uamuzi wa kukamatwa kwa Mahela umetolewa jana Jumatatu Septemba 9, 2019, na Lugola baada ya kufanya ziara katika kanisa hilo kufuatia malalamiko ya mara kwa mara kutoka kwa majirani.

Amesema majirani wa eneo hilo kwa nyakati tofauti wamekuwa wakilalamikia kelele zinazotoka kanisani  hilo na licha ya viongozi wa serikali kumpa onyo la kujirekebisha mchungaji huyo lakini hakufanya hivyo.

“Ulikuwa ukiwaambia wananchi kuwa hujali na waende kokote leo kokote zimefika 40. Kokote nipo hapa na kokote hutopona,” amesema Lugola.


Loading...

Toa comment