Lugola Amwagiza Sirro Kumshughulikia Mbunge Aliyemtimua Polisi – Video

Baada ya kauli ya Mbunge Sophia Mwakagenda (CHADEMA) aliyosema leo asubuhi, Novemba 8, 2019 bungeni kuwa amemuondoa mpangaji ambaye ni Polisi kwenye nyumba yake kwa sababu haoni haja ya kushirikiana nae.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Kangi Lugola amemuagiza Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro kumchukulia hatua Mbunge huyo na wengine wanaotoa kauli zenye viashiria vya uvunjifu wa amani.

 

“Jeshi la Polisi Tanzania tumekwishajipanga kuhakikisha amani inakuwepo kuanzia urejeshwaji wa fomu, rufaa, kampeni mpaka uchaguzi wa serikali za mitaa na matokeo. Hakuna Mtanzania yoyote, kikundi ama chama cha siasa kitakachofanya fujo ama kuharibu mali watu wakati wa uchaguzi.

 

“Nina taarifa chama kimoja kimejiondoa kwenye uchaguzi, ni imani yangu kwamba chama hicho kinaweza kuwa na mpango wa kuvuruga uchaguzi. Ninawaambia kwamba, hakuna chama chochote cha siasa kitakachovuruga uchaguzi, tutatumia nguvu yoyote kuhakikisha hakuna uvunjifu wa amani.

 

“Kuna viashiria vya uvunjifu wa amani vimeanza kujitokeza kuanzia humu Bungeni kwa kuwafukuza wapangaji, nawasishangae tukianza kuchukua hatua,. Tutaanzia hapa Bungeni kuchukua hatua.

 

“Namuelekeza IGP Sirro kuanza kuchukua hatua kuanzia Mbozi na kwa Mbunge huyu (Sophia Mwakagenda) ambaye ameanza kuonyesha viashiria vya uvunjishu wa amani. Wasiijaribu serikali ya awamu ya Tano, tuko vizuri sana, kiberiti kimejaa njiti, wakitikisa kitawaka,” amesema Lugola.

 

“Mimi Sophia Mwakagenda sina mtendaji wala sijui kiongozi gani niishipo nitakaefanya nae kazi mpaka muweke mambo yenu sawa, pia leo namtoa kwenye nyumba yangu mpangaji wangu ambaye ni askari polisi akakae huko anakolipwa mshahara, nyumba ni yangu,” alisema Sophia.

 

Na Edwin Lindege

“MSIJARIBU KUTUTIKISA, TUMEJAAAA/NAAGIZA MHE. MBUNGE AKAMATWE”:WAZIRI KANGI LUGOLA


Loading...

Toa comment