The House of Favourite Newspapers

Lugola Aonya Kuhusu Ajali, Ataka Wakimbizi Kurejea Kwao – Video

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema alilivunja Baraza la Usalama Barabarani  kutokana na baraza hilo kukosa tija katika kudhibiti ajali hizo na kwamba atatangaza baraza jipya mwisho wa mwezi huu.
Lugola wameyasema hayo leo Ijumaa  akizungumza na wanahabari ofisini kwake, jijini Dar es Salaam aliposisitiza pia kwamba wamiliki wa magari mabovu yanayosababisha ajali watakamatwa na  kufikishwa mahakamani,
Pamoja na kutoa onyo kwa askari wanaokula rushwa, kushirikiana na majambazi  na kuwabambikizia makosa wananchi, amewataka pia wakimbizi kutoka Burundi kurejea nchini kwao akisema hali ya huko ni shwari.
Alizungumzia pia suala la uwezekano wa mabasi kusafiri wakati wa usiku ambapo alisema atazungumza na wadau wa usafiri kuhusu jambo hilo.
“Julai 31 nitakutana na wadau wa usafirishaji kuzungumza nao ili wanipe mtazamo wao juu ya jambo hili la kutembea usiku,” alisema.

Na Edwin Lindege | Global Publishers

BREAKING: Maamuzi ya LUGOLA Kuhusu MBWA Aliyepotea

Comments are closed.