LUGOLA: ‘Magufuli Mtoto wa Mungu, Wahuni Washindwe na Walegee’ – VIDEO

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amemwelezea Rais John Magufuli kuwa ni mtoto mwadilifu wa Mungu na kwamba watakaojaribu kumhujumu katika jitihada zake za kuleta maendeleo, hawatafanikiwa.

 

Lugola ameyasema hayo wakati wa  uzinduzi uliofanywa na Rais Magufuli wa   nyumba 20 za makazi ya Jeshi la Polisi katika eneo la Magogo mkoani Geita ambazo zinawakilisha nyumba nyingine 94 zilizojengwa nchi nzima.

 

Waziri huyo amewakumbusha wananchi kwamba Rais Magufuli   alipochukua nchi hii ili kuwaongoza Watanzania,  jambo la kwanza aliahidi kulinda amani, hivyo, waziri huyo aliwataka majambazi na wahalifu wote, mmoja baada ya mwingine, wajisalimishe na kutafuta shughuli mbadala za tija kwa taifa.

 

Kuelewa zaidi alichosema Lugola, tazama video hapo juu.


Loading...

Toa comment