The House of Favourite Newspapers

Luis Miquissone ni Habari Nyingine

0

KIUNGO wa Simba raia wa Msumbiji, Luis Miquissone, amefunguka kuwa baada ya kufanikiwa kufunga bao lake la kwanza msimu huu, amepania kufanya makubwa ndani ya klabu hiyo, ikiwemo kufunga mabao mengi zaidi na kucheza soka safi.

 

Luis ameongeza kuwa bao hilo alilofunga dhidi ya Biashara United kwenye mchezo uliochezwa juzi Jumamosi Uwanja wa Taifa, Simba wakishinda 3-1, limempa nguvu na kumuamsha kupambana zaidi ili kufunga mabao mengi na kuisaidia timu hiyo kuwa bora, kwa kuwa ndiyo kitu pekee kilichomleta Simba.

 

Luis alitua Simba wakati wa dirisha dogo la usajili akitokea UD do Songo aliyokuwa anacheza kwa mkopo, akitokea Mamelodi Sundowns inayoshiriki Ligi Kuu Afrika Kusini.

 

Akizungumzia kiwango chake, Luis alisema kuwa anafurahi kuanza vizuri maisha yake ndani ya Simba, lakini pia anafurahi kufanikiwa kufunga bao lake la kwanza, jambo ambalo limempa nguvu ya kuonyesha uwezo zaidi wa kucheza soka safi lakini pia kufunga mabao mengi, huku akifunguka kuwa hicho ndiyo kitu kilichomleta Simba.

 

“Kwanza nianze kwa kumshukuru Mungu na wachezaji wenzangu wa Simba kwa msaada mkubwa wanaonipa, lakini pia nafurahi kuona kuwa nimefanikiwa kufunga bao langu la kwanza ndani ya Simba, nipo hapa kuisaidia timu kufunga mabao na kupata matokeo mazuri.

 

“Nimekuja Simba kwa sababu hiyo, kwa hiyo bao hili limenipa nguvu ya kuongeza kiwango changu na kucheza soka safi, nitacheza soka safi kila mara na nitafunga mabao mengi kila itakapowezekana, nawashukuru mashabiki wa Simba kwa sapoti yao, watarajie kuona mambo mengi mazuri kutoka kwangu,” alisema Luis.

Leave A Reply