Kartra

Lukaku Amvulia Kofia Ronaldo

MSHAMBULIAJI  hatari wa Chelsea, anayewika kwenye timu yake ya Taifa ya Ubelgiji, Romelu Lukaku mwenye umri wa miaka 28, amemvulia kofia nyota mpya wa Manchester United, Cristiano Ronaldo.

 

Katika mahojiano maalum na Mtandao wa Goal Asia, Lukaku amewasihi mashabiki wa mpira wasimlinganishe na Ronaldo ambaye ni Mchezaji Bora wa Dunia mara tano.

 

Lukaku anasema; “Ronaldo ni mchezaji mkubwa duniani, siwezi kufanana naye, nahitaji kujifunza vingi kutoka kwake, ni mmoja kati ya wachezaji watatu bora ulimwenguni katika historia ya mpira.

 

“Siwezi kusema ni wa ngapi, lakini nafikiri yeye ni bora zaidi yangu…”


Toa comment