The House of Favourite Newspapers

LULU DIVA HATAKI KUSIKIA ALIKOTOKA

Tokeo la picha la LULU DIVA
Lulu Abass ‘Lulu Diva’

MWANADADA Lulu Abass ‘Lulu Diva’ ambaye kwa sasa anakimbiza kwenye gemu la Bongo Fleva na Wimbo wa Ona ambao amemshirikisha Rich Mavoko, amefunguka kuwa ukitaka kukosana naye basi mshirikishe kwenye masuala ya ‘u-video queen’, aliyokuwa anayafanya huko nyuma. Akipiga stori na Risasi Vibes, Lulu alisema kwamba akikumbuka baadhi ya mambo kwenye u-video queen, muda mwingine hutamani hata kulia.

“Kiukweli sitaki kusikia kabisa kuhusu mambo ya u-video queen, ni kweli ni mapito yangu na ndiyo huko nilikotoka, lakini kwa sasa ninaendelea na kuweka akili yangu yote kwenye muziki ninaoufanya na uigizaji huko ndiko ninafikiria zaidi. “Mtu unachukuliwa na kupewa kazi ya kupamba wimbo wa mtu kwa malipo kidogo, bado hicho kidogo chenyewe unakihangaikia na manyanyaso kibao,” alisema Lulu Diva

Comments are closed.