The House of Favourite Newspapers

Lulu Amrudisha Ray C kwa Mungu – Video

MSANII nguli wa Bongo Fleva, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amejikuta akilengwa na machozi baada ya kuangalia video iliyosambaa mtandaoni ikimuonesha Muigizaji wa Bongo Movie, Elizabeth Michael ‘Lulu’ akiimba kwaya kanisani na kucheza.
Ray C amedai kuwa video hiyo imemfanya akumbuke kipindi cha nyuma wakati alipopitia kwenye matatizo ya kuugua kwani kipindi hicho alikuwa ni mcha Mungu na alikuwa hakosi kanisani tofauti na sasa.
“Lulu nimeangalia hii video zaid ya mara kumi nahisi!mpaka machozi yamenilenga kwakweli!Sikumbuki lini nimeingia kanisani!“ameandika Ray C kwa kujutia kwenye ukurasa wake wa Instagram na kusisitiza kuwa amejifunza jambo kutoka kwenye video hiyo. Najiona mzima sasa na nasahau kuwa Mungu ni mkali! nimejifunza kitu kutoka kwako my dear! kikubwa sana. You Inspire Me…,” amemaliza Ray C.
Picha na video ya Lulu ikimuonesha mwenye afya nzuri akiwa Kanisani akicheza na waumini wenzake ilisambaa Jumatatu ya wiki hii. 
Tazama video yenyewe hapa chini ikimuonesha Lulu akicheza kanisani.

Comments are closed.