LULU DIVA AANIKA SIRI YA KUUCHA MUZIKI

B AADA ya tetesi kusambaa kuwa ameachana na muziki na kujikita kwenye tamthiliya, msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ameanika siri hiyo kuwa hajaukacha muziki moja kwa moja bali ameamua kuangalia fursa nyingine. Akizun-gumza na Showbiz Xtra, Lulu alisema kuwa kwa sasa wanamuziki wengi wameamua kuingia kwenye tamthiliya kwa kuwa inalipa.

“Wanamuziki kwa sasa tumeingia kwenye tamthiliya kwa kuwa inalipa tofauti na muvi na pia tumeamua kufanya hivyo ili tuweze kuirudisha kwa sababu sanaa ilikuwa inazorota kwa hiyo tumekuja kuweka amshaamsha ili kuiinua ndio maana unaona wanamuziki tunaingia upande wa filamu na si kwamba nimeacha muziki kikubwa niwaombe Watanzania waendelee kusapoti kazi zetu ili tuweze kuwapa vitu vizuri zaidi,” alisema. Lulu kwa sasa anacheza Tamthiliya ya Rebbeca inayorushwa kupitia Dstv.


Loading...

Toa comment