LULU DIVA ACHOMOA KUZAA, KUTELEKEZA MTOTO

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefunguka kuwa madai ya kuzaa mtoto na kumtelekeza kijijini kwao ni ya uongo na kwamba wabaya wake wameamua kumchafua.

 

Katika mazungumzo na paparazi wetu, Lulu alisema mbaya wake huyo anayemchafua haelewi lengo lake, lakini kamwe asingeweza kumtelekeza mtoto wake wa kumzaa.

 

“Jamani huyo aliyesambaza habari hajui ni kiasi gani ananitesa, hili suala limeniathiri sana. Imefikia mahali sasa wachumba wananikimbia. “Yaani ukipata mwanaume, akisikia tu ulitupaga mtoto huko kijijini, anakula kona ila walimwengu wana shida nyingi sana. Hawapendi maendeleo ya wenzao,” alisema Lulu Diva.


Loading...

Toa comment