Lulu Diva Achukia Utimu Kwenye Gemu

SEXY Lady kunako anga la Bongo Fleva, Lulu Abas ‘Lulu Diva’ amefunguka kuwa kwa upande wake anachukia sana mambo ya utimu hasa katika muziki.

Akibonga na Mikito Nusunusu, Lulu alisema kuwa yeye anapenda kusimama peke yake kama jinsi alivyo sasa kwani kuwa katika timu fulani haisaidii kitu kwa upande wake.

“Mara zote napenda kujiangalia mimi na kusimama mwenyewe kama hivi nilivyo kwa sababu sipendi na siamini mambo ya utimu katika muziki maana haisaidii kitu chochote zaidi ya jitihada za mtu binafsi, japo kuna watu ambao wanapenda mambo hayo ila kwangu ni tofauti,’’ alisema Lulu Diva, staa wa ngoma ya Come Again aliyomshirikisha Eddy Kenzo kutokea Uganda.

Toa comment