LULU DIVA AFANYA ‘BETHDEI’ KWA DUA

Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ 

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amesema kuwa aliamua kufanya ‘bethdei’ yake kwa kuomba dua tu kwa sababu anaamini hiyo ndiyo njia sahihi kuliko kufanya sherehe kwenye kumbi za starehe.  Akizungumza na Ijumaa Wikienda mwanamuziki huyo aliyesherehekea siku yake ya kuzaliwa juzikati alisema aliamua kufanya hivyo kutokana na ukweli kwamba, kwa maisha ya sasa kila jambo ni vyema kumshirikisha Mungu.

“Unajua nimekaa nimefikiria unafanya ‘bethdei’ ukumbini na mashoga lakini walewale ambao umekula nao na kucheza nao siku hiyo watakusema vibaya na kuondoka zao, lakini ukisoma dua kwa muumba wako ndio kila kitu, kwa sasa kila ninalofanya lazima nimshirikishe Mungu,” alisema Lulu Diva


Loading...

Toa comment