Lulu Diva Afungukia Kufulia

Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’.

 

BAADA ya kudaiwa kwamba kwa sasa amefulia ndiyo maana hata mbwembwe zake hazisikiki tena mjini, mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefunguka kuwa watu wanaomsema amefulia watakuwa hawamuelewi vizuri.

 

Akichezesha taya na Mikito Nusunusu, Lulu Diva alisema watu wanaodhani mtu akiwa anajinadi kwenye mitandao ya kijamii, basi ndiyo maisha yake ya kweli anayoishi, wanajidanganya hivyo kwa sababu hawaoni nikifanya hivyo kama mwanzoni ndiyo wanaona kafulia.

“Unajua watu wanapenda sana kudanganywa mitandaoni ndiyo maana macho yao yanaangalia wale wanaojionesha na vitu feki, lakini kama mtu ametulia watasema amefulia, hapo nashindwaga kuelewa kabisa, niwaambie tu sijafulia na siwezi kwa sababu ninajitambua,” alisema Lulu Diva.

Stori: Imelda Mtema

Loading...

Toa comment