Lulu Diva Akoshwa na Nyimbo za Marioo

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Lulu Abas ‘Lulu Diva’ amefunguka kuwa anapenda kusikiliza nyimbo za msanii mwenzake Omary Mwanga ‘Marioo’.

 

Akizungumza na gazeti hili, Lulu amesema kuwa kwenye wasanii ambao wanajua kuimba nyimbo za mapenzi, ni Marioo. Huwa anaweza kusikiliza nyimbo zake siku nzima bila kuchoka.

 

“Napenda sana kusikiliza nyimbo za Marioo, kwa sababu nilishawahi kutendwa kwenye mapenzi. Kwa hiyo huwa nikisikiliza napata faraja sana, kwenye redio yangu naweza kusikiliza nyimbo zake kutwa nzima,” alisema Lulu Diva.

Stori: Khadija Bakari

Toa comment