The House of Favourite Newspapers

Lulu Diva Ampa Dongo Dada’ke

BAADA ya kudaiwa kukwapua bwana wa dada’ke aitwaye Mamuu, sistaduu wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amemtupia dongo dada yake huyo kuwa ameachwa kutokana na mapungufu aliyonayo.

Akizungumza na Amani, Lulu Diva alisema hadi mwanaume anaamua kutembea na mwanamke mwingine nje, ujue kuna shida mhusika atakuwa nayo hivyo anapaswa ajichunguze na ajirekebishe.

“Ningekuwa mimi ningeona aibu sana kutangaza mume wangu amechukuliwa na mwanamke mwingine, kwa nini aondoke kwako aje kwangu? Lazima utakuwa na tatizo,” alisema Lulu Diva.

Hivi karibuni mitandaoni kulichafuka kwa habari kuwa mwanamuziki huyo anatembea na mume wa dada’ke huyo, mtoto wa mama yake mkubwa. Jitihada za Amani kumpata dada mtu hazikuzaa matunda hivyo zinaendelea!

Stori: IMELDA MTEMA

Comments are closed.