The House of Favourite Newspapers

Lulu Diva Anasa Kwenye Penzi la Mzimbabwe!

 Lulu Abas ‘Lulu Diva’, katika moja ya picha zake alizopiga Global TV studio

Na Andrew Carlos | IJUMAA| ShowBiz

MWANAMUZIKI anayefanya poa kwa sasa katika Bongo Fleva na Ngoma ya Milele, Lulu Abas ‘Lulu Diva’ amenasa katika penzi la msanii kutoka Zimbabwe, Mukudzeyi Mukombe ‘Jah Prayzah’ na kwamba wawili hao wamekuwa wakijiachia bila wasiwasi.

Chanzo kiliitonya Showbiz kuwa, Lulu Diva aliyewahi kuwa video queen kwenye video mbalimbali na kuacha, amekuwa akisafiri mara kwa mara kwenda Zimbabwe na hata msanii huyo huwa anakuja kwa siri nchini.

Lulu Diva, akiwa na Mzimbabwe wake, Jah Prayzah.

“Mapenzi yao hayana kificho kwani Lulu kwa sasa ameamua kuachana na mapenzi ya Kibongo ambayo anaona kama ni ya kitapeli,” kilisema chanzo. Showbiz baada ya kunasa picha za wawili hao, ilimtafuta Lulu na kumhoji juu ya ishu hii ambapo alifunguka:

“Hizo habari kama unavyosikia ndiyo hivyo. Kwa sasa nimeamua kutulia na Jah (Prayzah) wangu na mbali na uhusiano, amekuwa akinionesha njia nzuri za kimuziki,” alisema Lulu.

Jah na Lulu kwenye ‘Insert’ wanapokuwa waki chat on line

Jah Prayzah anatamba na Wimbo wa Watora Mari aliomshirikisha staa wa muziki, Diamond Platnumz.

Shinda Nyumba Awamu ya Pili Yatikisa Jiji la Dar es Salaam

Save

Save

Comments are closed.