visa

Lulu Diva Anasa Mimba, Aibua Utata!

MAMBO ni moto! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mwanamuziki wa Bongo Fleva, Lulu Abass ‘Lulu Diva’ kukiri kunasa ujauzito lakini baba wa mtoto mtarajiwa kuzua utata, Risasi Mchanganyiko linakupa habari kamili. 

 

Chanzo makini kililieleza Risasi Mchanganyiko kuwa, Lulu Diva kwa sasa ni mjamzito lakini amechanganyikiwa kwani inasemekana ujauzito huo ni wa staa mkubwa hapa Bongo lakini mwenyewe amekuwa akificha sana huyo baba mtarajiwa.

 

“Lulu Diva ana mimba kama hamjui ndiyo nawapa habari hiyo, baba kijacho mtarajiwa ni utata mtupu maana anasemekana ni staa mkubwa, yaani mambo yamekorogeka vibaya,” kilisema chanzo hicho. Risasi Mchanganyiko lilimtafuta Lulu Diva ambaye alikiri kuwa na ujauzito lakini siyo wa msanii wala staa ni wa mwanaume mwingine nje ya sanaa.

Lulu Diva alisema anashangaa sana kusikia hizo habari za kwamba ujauzito wake ni wa staa mkubwa hapa Bongo kwani amepewa na mtu mwingine kabisa.“Jamani huu mji una mambo sana kila kukicha mambo yanazuka tu, hebu watu waniache na mimba yangu maana ni ya jamaa mwingine kabisa wasije wakafanya nikasusiwa matunzo ya mtoto bure,” alisema Lulu Diva.
Toa comment