Lulu Diva Atamba Kuwa Mama Bora

SEXY Lady wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ ametamba kuwa yeye ni mama bora (wife material), tofauti na watu wanavyomuona.

Lulu Diva anasema, yeye ni binti anayejua wajibu wake na pia siyo mtu wa kutumia pesa hovyo kwenye starehe kama ilivyo kwa mastaa wengine.

Akipiga stori na OVER ZE WEEKEND, Lulu Diva amesema, anamshukuru mama yake kwa kumfundisha jinsi ya kupambana na maisha, lakini pia kujua lipi jema na lipi siyo jema.

“Mimi nikiwa na njaa, napika nyumbani kwangu, siyo kwenda kununua mahotelini. Hayo maisha mimi sina, ukiona nimefanya hivyo, ujue ni mara chache mno na kuwe na sababu,” anasema Lulu Diva anayefanya poa na ngoma yake mpya ya Come Again aliyomshirikisha Eddy Kenzo wa Uganda.

STORI: MEMORISE RICHARD

Toa comment