Lulu Diva: Corona Imetutia Akili Wasanii

STAA wa muziki wa Bongo Fleva ambaye anakimbiza na ngoma ya Come Again, Lulu Abas ‘Lulu Diva’, amefunguka kuwa janga la Corona limewafundisha wasanii kuwa na akili ya kuweka akiba.

Akibonga na Risasi Vibes, Lulu amesema kuwa, wasanii huwa wanalemaa katika kuweka akiba kwa kutegemea kuwa muda wowote anaweza kupata shoo ya kufanya na kupata pesa ya kumsaidia, kumbe kuna umuhimu wa kuweka akiba pia.

“Wasanii tumepitia kipindi kigumu cha janga la Corona, tumefundishwa kuweka akiba na kuwa na matawi ya kutengeneza pesa zaidi, ukijua labda kuna kazi ambayo utafanya tu na kurudisha pesa iliyotoka, kumbe kuna kuweka akiba pia.

 

Sasa kwa kuwa kazi zilisimama kwa sababu ya janga hili, tukajifunza kabisa hata matumizi ya pesa,’’ alisema Lulu Diva huku akimpongeza Rais Dk John Magufuli kwa kuruhusu kazi ziendelee ikiwa ni baada ya kupungua kwa makali ya Virusi vya Corona.

Toa comment