The House of Favourite Newspapers

LULU DIVA KUFUNGUA KITUO CHA WATOTO YATIMA

 

Lulu Abbas ‘Lulu Diva’

BAADA ya Muziki wa Bongo Fleva kuonekana kumuendea sawa, hitmaker wa Ngoma ya Ona aliomshirikisha Rich Mavoko, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amesema kuwa yupo mbioni kufungua kituo cha watoto yatima.

 

Akizungumza na Star Showbiz, Lulu Diva alisema kuwa, amekuwa akiguswa sana na maisha ya watoto wanaoishi katika mazingira magumu ambao hawana baba wala mama hivyo akaona kwenda kutoa tu misaada mara kwa mara kwenye vituo vyao haitoshi bora kufungua kituo chake kitakachowasaidia.

 

“Nimefuatilia taratibu zote za kufungua, kiwanja kipo maeneo ya Tegeta hivyo ni muda muafaka kuwasaidia watoto yatima wanaoishi katika mazingira magumu,” alisema Lulu Diva ambaye anawafunika mastaa wengi wa kike Bongo kwa kutembea na gari la thamani aina ya Jeep Wrangler.

ANDREW CARLOS

Comments are closed.