The House of Favourite Newspapers

Lulu Diva: Ningekuwa Mdangaji, Ningezeeka

0

Msanii wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amefunguka kuwa kama angekuwa mdangaji kama watu wanavyosema basi angeshazeeka siku nyingi kwa sababu sio lazima mtu akiamka kitandani aanze kufikiria wapi pakwenda kudangia ingekuwa ni shida sana kwake.

Akizungumza na MIKITO NUSUNUSU, Lulu Diva amesema kuwa watu wanachukulia poa tu kudanga kumbe hawajui kudanga ni kujizeesha na msichana mwenyewe maisha yake mazuri ni ngumu sana kufanya mambo hayo.

 

“Hivi ningekuwa mdangaji si ningeshazeeka mapema watu wanachukulia poa kudanga eeeh, hebu waniache kwanza niendelee na mambo yangu mengine mimi nina vitu vingi sana vya kufanya,” alisema Lulu Diva

STORI:IMELDA MTEMA , RISASI

Leave A Reply