Lulu Diva: Uno Langu Halijamsumbua Tanasha

BAADA ya kutunza fedha nyingi na kukata mauno ya aina yake kwenye arobaini ya mtoto wa mwanamuziki Nasibu Abdul ‘Diamond’ mwanamuziki Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ amesema uno lake alilokuwa akimkatia mwanamuziki huyo halijamshtua Tanasha bali watu wanatengeneza maneno.

 

Lulu Diva aliiyambia Wikienda kuwa alicheza kawaida sana lakini hajui kwa nini watu wamemchukulia kama alikuwa akicheza vibaya mbele ya Diamond.

 

“Sijui kama Tanasha anaweza kushtushwa na uno langu kwa sababu ni la kawaida sana na nilicheza tu siyo kwa ajili ya kumtega Diamond kama wanavyosema, wasinigombanishe na Tanasha,” alisema Lulu Diva.

STORI: IMELDA MTEMA

Toa comment