The House of Favourite Newspapers

LULU DIVA: HAKUNA MWANAUME KAMA IDRIS

Lulu Abbas ‘Lulu Diva’

MSANII wa Bongo Fleva, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’ juzikati amefunguka kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika kuwa, hakuna mwanaume mzuri kama Mshindi wa Big Brother 2014, Idris Sultan. 

 

Baada ya kuona posti yake hiyo, Showbiz Xtra ilimvutia waya mrembo huyo kumtaka afafanue zaidi kuhusiana na posti yake hiyo ambapo alipopatikana, alisisitiza kwamba, ameamua kuandika maneno hayo kwa sababu kaka yake huyo ni handsome (mzuri) na uzuri wake hauwezi kuufananisha na mwanaume mwingine yeyote Bongo.

“(Anacheka) ndio ni kweli nimeandika hivyo kwenye akaunti yangu ya Instagram kwa sababu Idris ni handsome jamani kwani we huoni? Halafu kila siku mi’ huwa namw-ambia hata tukio-nana sema nikaona haamini ndio maana nikaposti kuonesha msisitizo,” alisema Lulu Diva. Lulu Diva na Idris ni ndugu kwa maana ya mtoto wa baba mkubwa kwa baba mdogo.

Comments are closed.