Lulu: Nimepata Mume Anayenisikiliza, Hajawahi Kunipiga – Video
Mwigizaji Elizabeth Michael almaarufu Lulu na mama watoto wawili, akiwa ni mke halali wa Francis Sizza amefunguka kuwa mumewe huyo anamuelewa vizuri na anamsapoti kwenye kazi yake tofauti na watu wanavyoweza kuhisi.
Ameongeza kuwa hata mumewe alipohoji kwenye mitandao ya kijamii akitaka kujua nini huwa kinafanyika kwenye ‘scene’ za kitandani, ilikuwa ni masihara na hakuwa amemaanisha alichokisema.