Lulu, Wolper watangaziwa kichapo na Husna Maulid

husna (1)Video Queen wa Bongo, Husna Maulid.

Imelda Mtema
Video Queen wa Bongo ambaye pia aliwahi kushiriki Miss Tanzania 2011, Husna Maulid amewatangazia kichapo kwa mastaa wawili wa Bongo Muvi, Jacqueline Wolper na Elizabeth Michael ‘Lulu’ endapo watathubutu tena kumsogelea mpenzi wake wa sasa (jina kalificha).

LULU567Staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Akizungumza na Ijumaa hivi karibuni Husna ambaye pia amejikita kwenye ujasiriamali alisema kuwa, wakati f’lani yeye na Lulu walizinguana kwa sababu ya mwanaume aliyekuwa akifahamika kwa jina la Seki, akawa mpole, wakati mwingine akazinguana na Wolper kwa mwanaume Mkongo aitwaye Radjab Mwami, kwake pia akazidiwa nguvu, akakaa pembeni, sasa amemnasa mwanaume huyo na hataki ugomvi na mtu.

wolper1131.jpgStaa wa Bongo Muvi, Jacqueline Wolper.

“Nimekuwa mvumilivu sana kipindi cha nyuma lakini sasa hivi atakayethubutu kuniwangia nitamshushia kichapo, maneno haya yawafikie hao watu,” alisema Husna.
Ijumaa lilimtafuta Wolper kuzungumzia mkwara huo alipopatikana alisema: “Mimi nafikiri Husna bado ni mtoto, yaani hajakua kwa maana angekuwa ni mtu mzima na akili zake asingeongea mambo hayo.”
Lulu hakupatikana kupitia simu yake ya mkononi.


Loading...

Toa comment