The House of Favourite Newspapers

Lungi Adaiwa kumuingiza Q-Chillah Kwenye ‘Unga’

0
Staa mkongwe wa filamu Bongo, Lungi Mwaulanga.

NA MWANDISHI WETU | RISASI | HABARI

Staa mkongwe wa filamu Bongo, Lungi Mwaulanga amedaiwa kuwa ndiyo chanzo cha Mwanamuziki Shabani Katwila ‘Q-Chillah’ kuingia kwenye matumizi ya unga kabla ya hivi karibuni kuamua kuacha, Risasi Jumamosi limetonywa. Chanzo makini cha habari hii kilidai kuwa, Lungi alikuwa akijihusisha na madawa ya kulevya kwa njia ya kuuza ndiyo sababu kuu ya Q-Chillah kuingia kwenye madawa kwani alikuwa karibu naye muda mwingi.

Mwanamuziki Shabani Katwila ‘Q-Chillah’ .

“Hivi mnajua kuwa aliyemuingiza kwenye dawa za kulevya Chillah ni Lungi? Alikuwa anapika na kupakua naye na hapo ndipo Q-Chillah alipoanza kutumia unga maana Lungi alikuwa akiuza,” kilidai chanzo hicho.

Baada ya ubuyu huo kumwagwa, waandishi wetu walimsaka Lungi ambaye katika kulifungukia hilo alisema: “Kwanza unaniambia habari za nyuma sana, mimi nimuingize Q-Chillah kwenye madawa kwa sababu gani? Kama biashara hiyo nilifanya zamani, kuhusu mapenzi mimi siyajui mambo hayo namjua kama mwanamuziki niliyewahi kuwa naye karibu,” alisema Lungi.

Waandishi wetu pia walifanikiwa kuzungumza na Q-Chillah kuhusiana na madai hayo ya kuingizwa kwenye ‘unga’ na Lungi, hiki ndicho alichokisema: “Sipendi kukumbushiwa mambo hayo kabisa kwani ilikuwa ni ujana tu na huyo Lungi msimuingize kabisa kwenye mambo hayo, namheshimu sana.”

Leave A Reply