Lungi amlipua masogange

Msanii wa siku nyingi kwenye anga la filamu Bongo, Lungi Maulanga.

Gladness Mallya na Hamida Hassan

MSANII wa siku nyingi kwenye anga la filamu Bongo, Lungi Maulanga amemlipua Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’ kwamba hajui kutumia umbo lake vizuri ndiyo maana amemtelekeza mwanaye.Akipiga stori na Ijumaa, Lungi alidai Masogange amemwacha mwanaye kwa shangazi yake huku malezi yake yakiwa duni wakati yeye akijiachia kimjini.

 

 Video Queen, Agnes Gerald ‘Masogange’.

“Masogange ananichefua kwa kuwa amemtelekeza mwanaye, mimi nina watoto watatu na ninahakikisha wanasoma shule nzuri sasa yeye huyo mtoto mmoja tu anamshinda, anamsomesha shule za kayumba, inakuja kweli hiyo?
“Halafu Mungu amemjalia kuwa na umbo zuri, sasa angekuwa analitumia vizuri angeshindwa kumlea mwanaye katika mazingira mazuri mpaka akamwache kwa shangazi wake. Mbaya zaidi hata gari zuri hana, sasa umbo lake linamsaidia nini?” alisema Lungi.

 

Baada ya paparazi wetu kumsomea mashtaka Masogange, mrembo huyo alisema: “Mwanangu nilimpeleka kwa baba yake, kama ingekuwa nimemwacha kwa marafiki au sehemu nyingine hapo ningeambiwa nimemtelekeza, kuhusu mafanikio yangu siwezi kutangaza kwamba nina hiki au kile.

“Gari ni kitu cha kawaida sana, kitu cha maana ni nyumba sasa siwezi kuanika mambo yangu. Kuhusu umbo zuri huyo dada alitaka nijiuze? Siwezi kufanya biashara chafu mimi.”

JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS!


Loading...

Toa comment