Lungi, Ferguson wanaswa

Rapa Saulo John ‘Ferguson’ akiwa na  Lungi Maulanga.

Issa Mnally

Rapa mahiri wa bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa ya jijini Dar es Salaam Saulo John ‘Ferguson’ mwishoni mwa wiki iliyopita alinaswa na Lungi Maulanga wakiwa katika hali tete ndani ya Ukumbi wa Mango Garden.

Akiwa ameongozana na mkewe aitwaye Rose Bushoke kwenye onesho la Bendi ya African Stars ‘Twanga Pepeta,’ Ferguson aliteta na muigizaji huyo kila mkewe huyo alipokuwa akienda msalani na mara kadhaa walionekana wakishikanashikana kwa namna ya kuibua maswali.

Lungi alikuwa amekaa na kundi la marafiki zake waliokuwa meza iliyo jirani na mwimbaji huyo wa zamani wa Twanga Pepeta na marafiki zake walionekana kufurahia vitendo hivyo vilivyokuwa vikifanywa na wawili hao, ingawa alipozungumza na mwandishi wetu, aliomba kutochapishwa kwa picha zake.

Loading...

Toa comment