The House of Favourite Newspapers

Lungi Sasa Ateswa Na Serengeti Boys

 

lungi-1

Msanii mkongwe kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Lungi Mwaulanga akiweka sawa nyumba yake anaishi Kinondoni jijini Dar.

KAMA ilivyo ada ya kolamu hii, huwa inatimba nyumbani kwa mastaa mbalimbali na kuangalia mazingira wanayoishi majumbani mwao ambapo leo tunaye msanii mkongwe kwenye tasnia ya filamu za Kibongo, Lungi Mwaulanga, ambaye anaishi Kinondoni jijini Dar.

Mpaka Home: Mambo, unaishi na nani humu?

Lungi: Poa! Naishi peke yangu ila kuna dada huwa anakuja kunisaidia kazi na kuondoka.

lungi-3

…Akiangalia TV.

Mpaka Home: Kwa hiyo wewe hujishughulishi na chochote hapa nyumbani hadi huyo msichana wa kazi aje?

Lungi: Hakuna kitu kama hicho, mimi ni mwanamke mchapakazi, kuna muda nafanya kazi zote mwenyewe, mara chache nikiwa ‘bize’ ndiyo huwa namuita.

Mpaka Home: Kwa hiyo ukiwa nyumbani unapendelea kufanya shughuli gani na starehe yako kubwa ni ipi?

lungi-5

Akiwa katika pozi.

Lungi: Nafanya kazi zote zinazostahili kwa mwanamke likiwemo suala zima la usafi na mapishi na starehe yangu kubwa ni kutazama muvi, naweza kuangalia hata siku nzima.

Mpaka Home : Najua una watoto, kwa nini huishi nao?

Lungi: Mungu hamtupi mja wake bwana, watoto wangu wote wanasoma shule za ‘boarding’ watatu hapa nchini na mmoja yupo Malaysia tena shule za bei juu, hivyo nakuwa nao kipindi wakija likizo tu.

Mpaka Home: Unapata wapi fedha za kuwasomesha hizo shule za gharama, maana siku hizi sikuoni kwenye filamu wala maigizo?

Lungi: Mpenzi wangu anawalipia, pia mimi kuna biashara nafanya ili nisife njaa, muda mwingine naandaa shoo za bendi ambazo kwa kiasi kikubwa huwa zinanisaidia kuishi vizuri.

Mpaka Home: Uliwahi kuandamwa na skendo ya kuwauza mastaa, vipi wewe ulishawahi kujiuza kwa hayo madanga?

img_0926

Akifuta vyombo vumbi.

Lungi: Hahaa, sijawahi kujiuza, mimi nilikuwa nawapa mchongo tu wenzangu na kama iliwahi kutokea hivyo sina kumbukumbu hiyo.

Mpaka Home: Una mkakati wowote wa kuingia kwenye maisha ya ndoa?

Lungi: Ndoa ni mipango ya Mungu, wakati ukiwadia basi huwezi kupingana na muumba, hivyo nashindwa kuongelea hilo ila wakati ukiwadia mtashuhudia.

 lungi-6

Muonekano wa nyumba anayoishi Lungi Mwaulanga.

Mpaka home: Ni kitu gani ambacho kinakukwaza kwenye maisha yako?

Lungi: Tabia ya mashabiki kunisumbua mtandaoni hainivutii hata kidogo, wengine ni watoto wadogo mno kwangu lakini wanakosa heshima najisikia vibaya sana, sababu najiheshimu mno isitoshe nawachukia mno Serengeti Boys.

Mpaka Home: Nimezoea kukuona ukivaa mavazi ya Kizungu, leo nakuona ndani ya dera, kulikoni?

Lungi: Si unajua hapa niko nyumbani tu wanaweza kuja wageni wa aina mbalimbali lazima nijisitiri, pia umri unaenda siku hizi napenda sana kujisitiri.

Mpaka Home: Haya nashukuru, ahsante kwa ushirikiano.

Lungi: Ahsante kwa kuja, karibu tena.

Comments are closed.