The House of Favourite Newspapers

Lungi: Skendo ya kuwauza mastaa iliniumiza!

0

lungiHII ni safu mpya itakayokuwa ikiwafuata mastaa popote walipo na kufanya nao mahojiano mafupi juu ya mishemishe zao za hapa na pale. Kwa kuanza, leo tunaye msanii wa filamu Bongo, Lungi Mwaulanga.

Mwanadada huyo alifumwa na paparazi wetu akila bata Picolo Beach and Hotel iliyopo Kawe jijini Dar es Salaam.

Mwandishi: Mambo vipi?

Lungi: Poa, nambie.

Swali: Naona unakula maisha, hivi ratiba yako kwa siku ikoje?

Lungi: Inategemea na siku, wakati mwingine nashinda nyumbani naangalia movie.

Swali: Viwanja vyako vya kujiachia na kula bata ni vipi?

Lungi: Mara nyingi huwa napenda kuja hapa Picolo, Serena na Jangwani Sea-Cliff, hizo nd’o sehemu kubwa napenda kwenda kutuliza akili.

Swali: Nini kinachokuvutia zaidi sehemu hizo na starehe yako kubwa ni ipi?

Lungi: Navutiwa na mazingira yake, yametulia sana na starehe yangu kubwa ni kuogelea. Naamini ni mazoezi tosha, kwa wiki lazima niogelee walau mara mbili, nisipofanya hivyo nahisi kuugua, pia Ijumaa napenda kwenda Serena huwa wanapiga live band.

Swali: Ukienda kula bata huwa pamoja na shemeji?

Lungi: (Kicheko) mara nyingi huwa na rafiki yangu anaitwa Mariam, shemeji yako yupo bize, siyo mtu wa kujiachia sana.

Swali: Ukiwa kama mtu maarufu watoto wako umewajenga kwenye misingi ipi na unaishi nao au?

Lungi: Wanangu wanaishi kawaida sana, sitaki kuwaanika kwenye media kama walivyo mastaa wengine, wote watatu wanasoma boarding na wa mwisho anasoma Malaysia.

Swali: Kwa nini uliamua kujiweka kando na sanaa na unajishughulisha na nini kwa sasa?

Lungi: Sasa hivi nafanya biashara pia ni promota, huwa nakodi bendi na kuandaa shoo, niliacha sanaa kutokana na malipo madogo, kipindi naigiza ulikuwa unalipwa 50,000 au usilipwe kabisa. Nina mpango wa kuanza kuandaa movie zangu na kuzipeleka sokoni lakini si kuigiza.

Swali: Ulishawahi kutafunwa na skendo ya ukuwadi kwa kuwauza mastaa kwa wenye nazo, unajisikiaje ukikumbuka hiyo ishu?

Lungi: Huwa naumia sana moyoni, najiona nilikuwa nikimkosea Mungu, siku zote natubu kutokana na hilo.

Swalii: Shepu yako iko vizuri, unapata usumbufu gani kutoka kwa wanaume wakware?

Lungi: Usumbufu upo, kikubwa ni kujitambua na kujiheshimu.

Swali: Tunaona wasanii wengi wako kwenye ushindani wa kumiliki ndinga za maana, wewe ni usafiri gani unakunyima usingizi?

Lungi: Mmh mimi sipendi makuu, ila kuna gari linaitwa Posh, siyo siri linanitoa machozi kila nikiliona.

Swali: Mastaa wengi wa kike wanaendesha maisha yao kwa kutegemea wanaume, vipi wewe?

Lungi: Mimi sitegemei mwanaume kuzungusha gurudumu la maisha, napenda kula kitu ninachokipata kupitia jasho langu.

Leave A Reply