The House of Favourite Newspapers

Luteni Karama: Kolabo na Mfaransa imenirudisha upya

0

DSCN6749Mkongwe katika muziki wa Bongo Fleva, Luteni Karama.

Mwandishi wetu

MKONGWE katika muziki wa Bongo Fleva, Luteni Karama amefungukia kolabo aliyoachia hivi karibuni akiwa na staa wa muziki kutoka Ufaransa, Jerry Julian kuwa imemrudisha upya kwenye chati ya muziki huo.

Akizungumza na Amani, Karama alisema kuwa ngoma hiyo inayojulikana kwa jina la The Way I Feel imetokea kupendwa na mashabiki wake wengi na kudhihirisha hilo imepakuliwa zaidi ya mara laki moja kwenye mitandao mbalimbali hususan Youtube kwa muda mfupi tu.

“Nimeamua kuja kivingine. Si unajua siku hizi gemu imebadilika sana lazima ujiongeze na kuangalia mwelekeo kabla hujafanya chochote, ndiyo maana nikaamua kumshirikisha Jerry Julian ambaye kishafanya kazi kwenye majukwaa makubwa ya Ulaya kama Paris, Amsterdam, London na kwingineko,” alisema Karama.

JIUNGE NA GLOBAL BRAKING NEWS

GLOBALBREAKINGNEWS100.jpg

Leave A Reply