The House of Favourite Newspapers

Lwakatare ateuliwa kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu Mabasi ya DRT

0

drt SIMBACHAWENE (1)Mabasi yendayo haraka Dar.drt SIMBACHAWENE (2)Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Simbachawene.

TAARIFA KWA UMMA

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. George Boniface Simbachawene (Mb) kwa Mamlaka aliyopewa chini ya Kifungu cha 2(2) cha Amri ya kuanzisha Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART), (The Executive Agencies) (The Dar Rapid Transit Agency) (Establishment) Order ) Tangazo la Serikali namba 120 la 2007, amemteua Mhandisi Ronald Lwakatare kuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Dar es salaam (DART) kuanzia tarehe 04/01/2016.

Uteuzi huo unafuatia kusimamishwa kazi kupisha uchunguzi kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu Bibi Asteria L. Mlambo tarehe 23/12/2015. Kabla ya uteuzi huu, Mhandisi Ronald Lwakatare alikuwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mfuko wa Barabara (Road Fund Board) akishughulikia Ufuatiliaji na Tathmini. Mhandisi Lwakatare anatakiwa kuripoti na kuanza kazi mara moja.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini cha Ofisi ya Rais – TAMISEMI, Januari 05, 2016

Leave A Reply