The House of Favourite Newspapers
gunners X

Lwandamina Amaliza Mchezo kwa Wasomali

0

KOCHA Mkuu wa Azam, George Lwandamina, ameweka wazi kuwa wana matumaini makubwa ya kupata matokeo mazuri katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Horseed ya Somalia, ili kujiandaa na mchezo wa raundi ya kwanza ya michuano hiyo.

 

Lwandamina Jumamosi iliyopita aliwaangoza Azam kushinda mchezo wa kwanza wa michuano hiyo hatua ya awali baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Horseed.

 

Jumamosi hii, Azam watarudiana na Horseed ambapo mshindi wa jumla atafuzu hatua ya kwanza ya michuano hiyo. Mechi zote mbili zinachezwa Uwanja wa Azam Complex, Dar.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Lwandamina alisema: “Wikiendi iliyopita tulikuwa na mchezo mzuri wa mkondo wa kwanza dhidi ya Horseed na kupata ushindi ambao sasa unatupa kujiamini kuelekea mchezo wa marudiano utakaofanyika Septemba 18, mwaka huu.

 

“Tulikuwa na muda mwingi wa mazoezi magumu ya utimamu wa mwili, lakini kwa sasa tunafanya mazoezi ya kimbinu zaidi, matumaini yangu kuwa tutafanya vizuri katika mchezo huo ili kuanza kujiandaa na hatua ngumu inayofuata.”

 

Bouteflika aliongoza nchi hiyo kwa karibu miongo miwili na kuachia madaraka mwaka 2019 baada ya jaribio lake la kugombea muhula wa tano kusababisha maandamano makubwa.

JOEL THOMAS NA INESS LUAMBANO, Dar es Salaam

 

Leave A Reply