Lwandamina Amfungulia Milango Straika Yanga SC

KOCHA Mkuu wa Yanga, Mzambia, George Lwandamina amemruhusu straika wake, Matheo Anthony kuondoka klabuni hapo ili akatazame maisha sehemu nyingine baada ya kuona hatakuwa na nafasi ya kumtumia tena msimu ujao.

 

Matheo ambaye alijiunga na Yanga misimu mitatu nyuma akitokea KMKM ya Zanzibar, hana nafasi yake ya kucheza kwenye kikosi cha timu hiyo kutokana na wingi wa washambuliaji.

 

 

Kwa sasa kuna uwezekano mshambuliaji huyo akatimkia Lipuli FC ya Iringa kutokana na klabu hiyo kuonyesha nia ya kumhitaji. Kikizungumza na Championi Jumatano, chanzo makini kimesema kuwa ombi la Matheo limekubaliwa hivyo msimu huu hatakuwepo tena Yanga hadi pale mambo yatakapomnyookea huko aendako endapo atafanya vizuri kiasi cha kumshawishi tena kocha kumrudisha kikosini hapo.

 

“Lwandamina amemruhusu Matheo kuondoka na wenzake wengine watano ambao ni Yusuf Mhilu, Baruan Akilimali, Juma Mahadhi, Maka Edward na Saidi Makapu, kocha kaona awaruhusu wote ili aweze kuangalia safu nyingine itakayokuwa na uwezo wa kutumika tofauti na ilivyo sasa ambapo wengine wanaonekana kushindwa kumudu kasi yake,” kilisema chanzo hicho

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment