Lwandamina Awaita Fasta Mastaa Wake

KOCHA Mkuu wa Azam FC, George Lwandamina,amekirejesha kikosi chake kambini haraka baada ya kuwapa mapumziko ya siku moja.

 

Wikiendi iliyopita Azam ilitoka suluhu na Pyramid ya Misri kwenye mchezo wao wa hatua ya kwanza ya Kombe la Shrikisho Afrika.

 

Azam itacheza na Biashara United octoba 19 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa nje kidogo ya Jiji la Dar, huku huo ukiwa mchezo wao wa tatu wa Ligi.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu Ofisa Habari wa Azam, Thabiti Zakaria amesema kuwa kocha wao amewataka wachezaji wote kufika kambini haraka.

 

“Mwalimu amewataka wachezaji warudi kambini kesho (leo), kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu na Biashara na baadaye mchezo wa marudiano na Pyramid, nafikiri anataka kuona wanajiandaa vyema kabla ya michezo hiyo,” alisema Zaka.

CAREEN OSCAR, Dar es Salaam2176
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment