The House of Favourite Newspapers

Lwandamina Vs Omong Rekodi Zinasema

0
George Lwandamina wa Yanga

LEO Jumamosi Yanga inaikaribisha Simba katika mchezo namba 58 wa Ligi Kuu Bara katika raundi ya nane ya ligi hiyo kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

 

Ni mchezo uliojaa tambo na matumaini ya kila upande kwani mambo mengi hadi sasa timu hizi zinalingana isipokuwa zimetofautiana katika mabao ya kufunga na kufungwa tu. Gumzo hasa ni ubora wa makocha wao, Joseph Omog wa Simba na George Lwandamina wa Yanga, hawa wote hadi sasa wamezipa timu zao ubingwa mmoja na msimu huu ndiyo utakaotoa jibu kwao.

 

Lwandamina ni raia wa Zambia aliyetua Yanga Desemba mwaka jana, lakini kazi rasmi alianza Januari mwaka huu, wakati Omog yeye ni raia wa Cameroon aliyeanza kuifundisha Simba msimu uliopita. Hebu tazama takwimu za makocha hawa;

Joseph Omog wa Simba

OMOG MBABE

Hadi sasa makocha hawa wamekutana katika mechi tatu ambazo Omog ameshinda zote, mechi hizo ni ile ya Kombe la Mapinduzi Januari 13, mwaka huu ambapo Simba ilishinda kwa penalti 4-2 baada ya suluhu.

 

Mechi ya pili ni ile ya Ligi Kuu Bara Februari 21, mwaka huu ambapo Simba ilishinda mabao 2-1 na ya mwisho ni ile mechi ya Ngao ya Jamii iliyochezwa Agosti 28, mwaka huu na Simba ikashinda kwa penalti 4-5, baada ya kutoka suluhu.

 

LWANDAMINA HOI

Mara zote wakati Simba inamfunga, Lwandamina ameonekana ni kocha mwenye mwono wa mbali zaidi na hatetereki na matokeo tofauti na yaliyo katika vichwa vya mashabiki wa Yanga. Anaonekana wazi mechi moja tu si tatizo kwake na anachojali ni mafanikio ya jumla ya Yanga kama kuchukua ubingwa.

OMOG HOI NJE YA DAR

Katika mechi tatu za ugenini, Omog amepata ushindi mara moja na kutoka sare mbili. Hii imeonyesha nguvu ya Simba nje ya Uwanja wa Uhuru ni ndogo kulinganisha na Yanga. Simba ilitoka suluhu na Azam FC, ikatoka sare ya mabao 2-2 na Mbao FC halafu ikaifunga Stand United mabao 2-1.

 

LWANDAMINA MKALI NJE

Katika mechi nne Yanga ilizocheza ugenini, imetoka sare moja na kushinda mara tatu. Yanga iliifunga Njombe Mji bao 1-0, ikatoka sare ya bao 1-1 na Majimaji, ikazifunga Kagera Sugar 2-1 na Stand United mabao 4-0.

OMOG ANAPATIA NYUMBANI

Katika mechi nne alizocheza nyumbani, Omog ameweza kupata ushindi mara tatu na sare moja. Alianza kwa ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya Ruvu Shooting, akaifunga Mwadui FC mabao 3-0, akatoka sare ya bao 1-1 na Mtibwa Sugar kabla ya kuifunga Njombe Mji mabao 4-0.

LWANDAMINA HAELEWEKI ‘HOME’

Ndani ya mechi tatu za nyumbani kwenye Uwanja wa Uhuru, Yanga imeshinda mara moja tu na kutoka sare mara mbili. Yanga ilianza kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Lipuli FC, ikaifunga Ndanda FC bao 1-0, halafu ikasuluhu na Mtibwa.

OMOG YUPO ‘MKIWA’

Katika benchi leo Omog anaweza kuwa na msaidizi wake Masoud Djuma kwa mara y a kwanza dhidi ya Yanga baada ya Jackson Mayanja kuamua kuacha kazi, hivyo ana msaidizi ambaye haifahamu Yanga vizuri kama ilivyokuwa katika mechi tatu zilizopita. Hii inaweza kumpa tabu kidogo.

LWANDAMINA FRESH TU

Katika mechi mbili za kwanza alikuwa na msaidizi wake, Juma Mwambusi lakini mechi moja iliyopita alikuwa na beki wa zamani wa Yanga, Shadrack N s a j i g w a na ndiye takayekuwa naye leo. Hapa kuna faida kwake kwani Nsajigwa anaifahamu vizuri Simba na baadhi ya wachezaji kama Haruna Niyonzima na Emmanuel Okwi amewahi kucheza nao, hivyo inaweza kuwa faida kwake.

Leave A Reply