Lwanga: Sichezi Rafu, Natimiza Majukumu Yangu

KIUNGO mkata umeme wa Simba, Mganda Taddeo Lwanga, ameibuka na kubainisha wazi kwamba yeye hachezi rafu kama wengi wanavyosema badala yake anakuwa anatimiza majukumu yake.

 

Kiungo huyo ameongeza kwamba, kwa nafasi yake kama kiungo mkabaji inabidi ajitume kwa ajili ya kulilinda lango lake ambapo kama angekuwa anacheza rafu angekuwa anatoka mchezoni.

 

Lwanga mara nyingi amekuwa akicheza soka la kutimiza majukumu yake ya kuhakikisha lango lao halipati kushambuliwa na wapinzani wao kwenye mechi zao za ligi kuu au Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mganda huyo ameliambia Championi Jumatano kuwa: “Hapana, hapana, mimi sichezi rafu, ila kama kiungo mkabaji natakiwa kuwa makini mchezoni muda wote. Kama ningekuwa nacheza hivyo ningekuwa natoka sana mchezoni, lakini sifanyi hivyo hata kidogo.

 

“Naisaidia timu kushinda mechi zake na hilo ndiyo jambo ambalo nalifanya mara zote, natimiza majukumu yangu kwa kulilinda vyema lang

Toa comment