The House of Favourite Newspapers

Lwanga: Tutawafunga Tena Al Ahly Kwao

0

KIUNGO Mkabaji wa Simba, Mganda, Taddeo Lwanga, amewasifu wapinzani wao Al Ahly ya Misri huku akitamba kuchukua pointi tatu mara watakaporudiana nyumbani kwao.

 

Hayo aliyasema mara baada ya kumalizika kwa mchezo wa hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika uliopigwa juzi Jumanne kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar na Simba kushinda 1-0.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Lwanga aliweka wazi siri ya ushindi huo kuwa ni umoja na ushirikiano waliokuwa nao kabla ya mchezo huo kuanzia kwa viongozi, benchi la ufundi na wachezaji.

Lwanga alisema kuwa katika mchezo huo waliingia uwanjani kwa lengo moja pekee la kuchukua pointi tatu, hiyo ndiyo sababu ya kucheza soka safi huku wakishambulia na kulinda goli lao kwa pamoja.

 

“Katika mchezo dhidi ya Al Ahly tulikuwa tunahitaji pointi tatu, tunashukuru tumezipata mbele ya mabingwa mara tisa wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Ni hisoria kubwa kwetu.”

Al Ahly ni timu nzuri kwenye ushambuliaji, tunawaheshimu nje ya uwanja ila ndani ni wachezaji 11 kwa 11 na leo (juzi) wachezaji wote tulikuwa vizuri na mwisho wa mchezo tukafanikiwa kuwafunga.

 

“Katika mchezo huu siri kubwa ya ushindi ni mbinu tuliyokuwa tunaitumia ya kucheza kwa nguvu ili kuhakikisha Al Ahly hawapati nafasi ya kucheza kutokana na ubora wa mpira wanaocheza,” alisema Lwanga.

STORI: WILBERT MOLANDI SAID ALLY, Dar

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Leave A Reply