The House of Favourite Newspapers

LYNN ALIKUWA NA KATABIA KA’ UDOKOZI! IMEFUNUKA

MUUZA nyago maarufu Bongo, Irene Godfrey ‘Lynn’ amefunua jinsi alivyokuwa anapen­da kula maziwa ya unga kiasi kwamba alikuwa anadiriki kudokoa pesa za mama yake ili mradi tu akanunue maziwa hayo.

 

Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Lynn al­isema alipokuwa mdogo alikuwa anapenda sana kulamba maziwa ya unga, ikawa asipoyapata ana­kosa amani hivyo alifanya kila awezalo apate pesa akayanunue.

 

“Yaani nilikuwa napen­da sana kulamba maziwa ya unga kiasi kwamba nilianza kuwa na katabia ka’ kudokoa pesa za mama ilimradi tu ni­pate maziwa ila ikafika wakati mama ikambidi azoee hiyo hali, akawa ananipa pesa nika­nunue ili nisizoee tabia ya wizi,” alisema Lynn.

Stori: Shamuma Awadhi

 

Steve Nyerere, MC Pilipili, Mwijaku Katika Usiku wa Chekelea Stand Up Comedy

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO


Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.