LYNN AMTIKISA TANASHA KWA MONDI

Irene Louis ‘Lyyn’

DAR ES SAAM: Msanii na video queen maarufu Bongo Irene Louis ‘Lyyn’ kwa mara ya kwanza amefunguka juu ya tetesi zinazosambaa mitandaoni kuwa amerudiana na zilipendwa wake Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ baada ya picha yake akiwa kitandani kwa msanii huyo kuvuja.  Akipiga stori mbili-tatu na Ijumaa mrembo huyo alisema kuwa anashangaa watu wanamsema vibaya uko mitandaoni kuwa amerudiana na Diamond wakati siyo kweli, kwa sababu mahusiano yake na msanii huyo yalishaisha kitambo.

“Mimi nashangaa watu walivyoniandama uko Instagram kuwa nimerudiana na Diamond, jamani siyo kweli mimi sipo na Diamond, hatujarudiana kabisa na wala hatuna mpango wakurudiana, halafu naomba waelewe kitu kimoja kwamba  kitanda hajatengenezewa Diamond peke yake vile vitanda vipo vingi kwa hiyo mtu yeyote ana uwezo wa kuwa nacho, kwa hiyo naomba waniache tafadhali nina maisha yangu mengine kabisa mbali na hayo wanayokesha kunisema kila siku,” alisema Lyyn.

Skendo ya Diamond kumsaliti mpenzi wake wa sasa Tanasha ilianza kusambaa hivi karibuni baada ya Lyyn kuposti picha mtandaoni akiwa kwenye kitanda ambacho inasemekana ni kitanda cha Diamond kwani hata Tanasha amewahi kupiga picha akiwa amekaa kwenye kitanda hicho, jambo lililowafanya mashabiki kuunganisha matukio na kumtaka Tanasha aachane mara moja na msanii huyo ili yasije yakamtokea ya Zari ambaye naye aliwahi kukuta hereni za mwanamke chumbani kwa Diamond


Loading...

Toa comment