Lynn: Ninachomisi kwa Mondi ni wivu

MREMBO aliyewahi kubanjuka penzini na staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Mondi’, Irene Hillary ‘Lynn’ ameweka wazi kuwa, kitu pekee anachokimisi kutoka kwa zilipendwa wake huyo ni wivu tu.

Lynn alifunguka hayo jana kwenye studio za +255 Global Radio zilizopo Sinza-Mori jijini Dar alipokuwa akifanyiwa mahojiano katika kipindi cha Bongo 255.

“Kitu pekee ninachomisi kutoka kwa Mondi ni wivu tu, jamaa ana wivu sana, labda hicho ndio kitu ambacho nakimisi,” alisema Lynn.

Mrembo huyo anayefanya Bongo Fleva, amezungumza mengi na +255 Global Radio, ili kuyapata waweza tembelea tovuti ya www.globalradio. co.tz.

Stori: Mwandishi Wetu, AMANI

Toa comment