Lyyn Atambulisha Nyimbo 2 Bongo 255 Ya Global Radio

Video Queen Bongo, Irene Godfrey Louis ‘Lyyn’ akifanyiwa mahojiano na Bongo 255.

VIDEO Queen Bongo, Irene Godfrey Louis ‘Lyyn’ leo Jumatano Oktoba 2, 2019 amefika katika mjengo wa Global Group kwa ajili ya kutambulisha ngoma zake mpya ‘Chomeka Kama Yote’ na ‘Pepea’ kwenye kipindi cha Bongo 255 kinachoruka kupitia +255 Global Radio ambapo amesema ametimiza miaka 20 tangu alipoanza kazi ya video Queen akiwa na miaka 18 tu.

Katika mahojiano yake, Lyyn alifunguka jinsi alivyokutana na memba wa Kundi la Wasafi Classic Baby ‘WCB’, Rayvanny kuwa mwanzoni alikuwa akisitasita lakini mwisho wa siku alifika katika studio za WCB ambapo wasanii hao walimpa moyo na kukubali kufanya kazi ya kwanza ya Kwetu ya msanii huyo akiwa kama video queen.

 

Mara baada ya kutambulisho ujio huo, Lyyn aliwaomba mashabiki waendelee kumsapoti katika kazi zake na ataendelea kutoa kazi bora ambazo zitawafurahisha mashabiki wengi wa muziki wa Bongo Fleva.

“Nawashukuru sana WCB kwani wao ndiyo walionifungulia milango ya mafanikio katika tasnia hii, pili nawashukuru mashabiki wote kwa kunipokea na nawaahidi sitawaangusha,” alisema Lyyn.

Lyyn (katikati) akiwa na watangazaji wa Bongo 255, kushoto ni Rashid Mbegani na Stewart George.

Mhariri wa Gazeti la Championi Ijumaa, John Joseph akiwa na Lyyn.

Mhariri wa Gazeti la Championi Jumamosi, Lucy Mgina akiwa na Lyyn.

Lyyn akisaini kitabu cha wageni muda mfupi baada ya kufika Global Group. Kulia kwake ni Meneja wa Global Radio, Borry Mbaraka.

Lyyn akiwa na Meneja wa Radio, Borry Mbaraka.

 

 

Toa comment