The House of Favourite Newspapers

M-BET yakabidhi mil. 17 mshindi michezo ya kubahatisha

0

M-BET (1)

Mkurugenzi wa M-BET Dhiresh Kaba (kushoto) akimkabidhi mfano wa hundi ya zaidi ya sh. milioni 17 Kiboko Isomba Samaki baada ya kubahatika kushinda kupitia moja ya michezo inayoratibiwa na kampuni hiyo.   Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Tarimba Abbas, akishuhudia zoezi hilo.

M-BET (2)

Mkurugenzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Tarimba Abbas, akiongea jambo mbele ya wanahabari kwenye makabidhiano ya hundi hiyo.

M-BET (3)

Mshindi wa milioni 17, Kiboko Isomba, akitoa neno la shukrani kabla ya kukabidhiwa hundi ya fedha  aliyojishindia.

M-BET (4)

…Akifurahi mara baada ya kukabidhiwa hundi hiyo.

M-BET (5)

Dhiresh Kaba (kushoto) akiwa katika pozi na Isomba baada ya kuhitimisha makabidhiano hayo ndani ya Ukumbi wa Samaki-Samaki Masaki jijini Dar es Salaam mapema leo.

M-BET (6)

Kaba (katikati) akiwa kwenye pozi la pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa M-BET.

KAMPUNI ya M-BET inayojishughulisha na michezo ya kubahatisha, mapema leo imemkabidhi Kiboko Isomba Samaki kitita cha shilingi milioni 17 za Kitanzania baada ya kubahatika kushinda moja ya michezo ya kubahatisha inayoratibiwa na kampuni hiyo.

Tukio la kukabidhiwa kwa fedha hiyo limefanyika mapema leo kwenye ukumbi uliopo katika baa maarufu ya Samaki-Samaki,  Masaki jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mbele ya wanahabari waliojitokeza kushuhudia makabidhiano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Tarimba Abbas, alisema kwamba Kiboko Isomba kutoka kijiji cha Bulamba Bunda mkoani Mara ni  mshindi wa pili kwa kujinyakulia kiasi kikubwa cha fedha kutoka kampuni hiyo.

“Nitumie fursa hii pia kuwapongeza M-BET kwa kuendelea kutoa fursa ya watu kulipatia taifa kodi zake bila usumbufu, kwani hapo awali baada ya Mwangasame kushinda sh. milioni 28 aliingizia serikali zaidi ya sh. milioni 6 kama kodi kupitia michezo hiyo,” alisema Tarimba Abbas.

Kwa upande wa mshindi wa bahati nasibu hiyo, Kiboko Isomba, amesema kwamba, anamshukuru Mungu kwa kumwezesha kushinda fedha hizo kwani alikuwa na ndoto za kuja kushinda siku moja, japokuwa amekuwa akicheza mara kadhaa bila kubahatika hadi leo hii ambapo ametumia shilingi elfu moja na kubahatika kuopata milioni 17.

“Fedha hii nina imani itanisaidia kutatua ndoto zangu za kuendelea kuchukua digrii ya pili katika Chuo Kikuu cha Makerere, Uganda, ambako nilikuwa nikisoma mwanzo na kukwama baada ya kuishiwa fedha za ada.

“Mimi ni mmoja wa Watanzania masikini na nimeshinda kutokea kijiji cha Bulamba, Bunda, Mkoa wa Mara, hivyo nafarijika sana kutoka kote huko na kuja hapa kupokea hundi hii ambayo inaenda kuendeleza ndoto zangu,” alisema Kiboko Isomba Samaki.

Habari/Picha: Musa Mateja/GPL.

 

 

  

 

Leave A Reply