The House of Favourite Newspapers

M-mama Kurahisisha Upatikanaji Wa Usafiri Wa Dharura Kwa Wajawazito Mkoani Songwe

0
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Mh. Happiness Seneda (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa chumba cha mfumo wa m-mama kurahisisha upatikanaji wa usafiri wa dharura ili kuokoa maisha ya wajawazito na watoto wachanga. Uzinduzi wa huduma ya m-mama ulifanyika katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe ikiwa ni ushirikiano wa serikali ya Tanzania, Vodacom Tanzania Foundation, Pathfinder, Touch Foundation na USAID. Pamoja naye ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe, Dkt. Boniface Kasululu.                                                                                               
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Mh. Happiness Seneda (wa kwanza kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa Mratibu wa M-mama Songwe, Aminiel Munisi wakati wa uzinduzi wa chumba cha mfumo wa m-mama kurahisisha upatikanaji wa usafiri wa dharura ili kuokoa maisha ya wajawazito na watoto wachanga. Kuanzia upande wake wa kushoto ni Mganga Mkuu wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Songwe, Dkt. Boniface Kasululu, Mganga Mfawidhi, Dkt. Lukombodzo Lulandala na Afisa wa Programu ya M-mama, Gladys Richard.                                                                                       
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Mh. Happiness Seneda akizungumza kwenye hafla hiyo.                          
Katibu Tawala Mkoa wa Songwe, Mh. Happiness Seneda na msafara wake walivyowasili eneo la tukio
Leave A Reply