Ma ex wa Diamond…Wanaigana au ni Madili Tu!

MASTAA wengi wa kike ni wahanga wa mitandao ya kijamii hasa kwa kupiga picha kali na kuzitupia katika kurasa zao mtandaoni, wengi wao wanavaa mavazi ya kuvutia na kupiga picha za aina tofautitofauti.  Kwa mastaa ambao ni wapenzi wa zamani wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond’ wao ndio wamekuwa wakitajwa sana kwa kushindana kwa mavazi na picha mbalimbali mtandaoni. Tumewaona Zarinah Hassan ‘Zari’, Hamisa Mobeto, Irene Louis ‘Lyyn’, Aunt Ezekiel, Wema Sepetu, Irene Uwoya na Jacqueline Wolper wakiwa wanachuana kwa kutupia picha za mvuto na kuzua gumzo kwani wanaonekana kuigana.

Pamoja na kuigana huko, wapo wanaodaiwa kuwa wanatangaza nguo mbalimbali za madukani na nywele lakini wakati mwingine ni mashindano tu. Kwenye makala haya leo tutaona jinsi mastaa hawa walivyoweza kupiga picha tofautitofauti ambazo zinafanana wakiwa kwenye vazi la bafuni kwa maana ya taulo na kikoti baada ya kuoga ‘house koti’.

WOLPER

Kwa mara ya kwanza kabisa alianza kupiga picha hiyo Wolper, ilikuwa ni siku ya kuzaliwa kwake ambapo alizipiga akiwa amejimwagia maua kibao lakini pembeni kukiwa na chupa za vinywaji.

Aunt Ezekiel

Haikuchukua muda mrefu Aunt Ezekiel naye alionekana akiwa amepiga picha kama hiyo ambapo alishika sabuni na kuibusu. Wapo watu waliosema anatangaza biashara lakini mara nyingine alionekana akiwa kwenye starehe zake na mpenzi wake ambapo alipiga picha hizo pia.

LYNN

Ni staa mwingine chipukizi aliyebanjuka na Diamond ambaye naye amewahi kupiga picha na vazi la bafuni na kutupia mtandaoni, ni vazi linalowapa mvuto wa aina yake.

UWOYA

Uwoya naye ni miongoni mwa mastaa ambao walionekana kuwa na vazi hilo ambapo haikujulikana kama anatangaza sehemu ya masaji au alikuwa nyumbani kwake.

HAMISA MOBETO

Mobeto yeye moja kwa moja alionekana akiwa anatangaza mafuta flani hivi ambapo alivaa vazi la taulo, alionekana amefanana pozi na hasimu wake Zarinah Hassan ambaye naye alipiga picha kama hiyo.

ZARINAH HASSAN

Ni miongoni mwa ma-ex wa Diamond ambaye alionekana kwenye vazi hilo la bafuni akiwa ameshika kinywaji ambapo wanazengo walionesha kuwa mwanamama huyo amemuiga Mobeto na kusahau kuwa vazi hilo ni mastaa kibao waliowahi kuwa kwenye uhusiano na Diamond wamependelea kupiga picha wakiwa kwenye vazi hilo.

Inasemekana wanaigana kila mmoja anataka kuonekana akiwa juu zaidi ya mwenzake lakini wapo wanaodai kuwa ni madili ya matangazo ambayo wanayapata ndiyo huwapa wazo la kufanana.

Mtu wa karibu na Mobeto alisikika akisema kuwa Mobeto si kama anamuiga mtu, isipokuwa wenye matangazo yao ndiyo humpangia pozi la kupiga picha. “Mobeto haigi mtu, watu wanaongea tu hayo ni mapozi kama mapozi mengine watangazaji wanaweza kuona kapiga mtu flani wakalipenda pozi na katika kuchagua wakamchagulia pia,” alisema Jamila, mmoja wa watu wa karibu na Mobeto.

Makala: Mwandishi Wetu


Loading...

Toa comment