The House of Favourite Newspapers

Ma-video queen wanavyotumika kama Big G

0

IMG-20151128-WA0016Gigy Money.

Wasanii wengi wa Muziki wa Bongo Fleva, kila wanapotoa nyimbo mpya hufikiria pia kuutengenezea video kali ili kuweza kuwashika vilivyo mashabiki zao. Katika video hizo, wapo wanaofikia hatua ya kwenda kuzifanyia nje ya nchi, hasa Afrika Kusini ambako wengi wanakimbilia huko.

Lakini sasa, kwenye uandaaji wa video hizo kuna watu muhimu sana ambao wamekuwa wakitumika kuzifanya ziwe na mvuto wa kutazamwa.

Watu hao ni wasichana wakali wanaofahamika kwa jina la Video Queens. Katika ulimwengu wa muziki wa sasa, wasichana hawa wana umuhimu mkubwa lakini sasa Kibongobongo inashangaza kuona baadhi yao wanatumika kama Big G.

Makala haya yana dhamira ya kuonesha mazingira magumu wanayofanyia kazi wadada hao. WANAPATIKANAJE? Zipo kampuni zinatoa ‘Mavideo Queen’ lakini wengi wanatoka mtaani tu.

12353809_1520170794943054_386606035_nKim Nana.

Wanachokifanya wanamuziki ni kutafuta wadada wazuri, wenye maumbile tata na wasio na aibu. Ndiyo maana ukifuatilia utabaini kuwa ‘Mavideo Queen’ wengi ni micharuko. Kama siyo mcharuko kazi hii huwezi kuifanya na kama utaifanya, itakuwa kwa shida sana.

MALIPO Nimejaribu kuzungumza na baadhi ya ‘Mavideo Queen’ wakanieleza kuwa, hawalipwi pesa nyingi kivile. “Unajua mimi niliwahi kulipwa shilingi laki moja tu tena kwa shida kucheza kwenye video ya….( anataja jina la mwanamuziki mkubwa). Nilikubali kwa sababu ya shida zangu.

Lakini kama hujui, Mavideo Queen wengine hawalipwi kabisa. Yaani wao ilimradi wauze sura na kupata umaarufu.

“Kwa mfano, wapo wadada ambao wako tayari kuonekana kwenye video za wasanii kama Ali Kiba, Dimpoz au Diamond bila hata malipo na wapo tayari kutumia gharama zao za mavazi, saluni ilimradi tu wauze nyago,” alisema mrembo mmoja aliyewahi kuonekana kwenye video nyingi za wa wasanii wakubwa aliyeomba hifadhi ya jina lake.

tunda2IYO KAZI YA KUITEGEMEA Wengi niliozungumza nao wanaeleza kuwa, U-video Queen una faida pale tu utakapobahatika kupata msanii akayekulipa vizuri na ukapata umaarufu wa kuweza kupata dili nyingine. “Kwa hapa mjini ukisema mimi kazi yangu ni u-video queen tu, unajidanganya.

Kwanza ukishaonekana kwenye video mbili tatu, tayari umechuja. Huwezi kupata dili tena. Ndiyo maana nasema ili uweze kuwa na maisha mazuri, fanya u-video queen na kazi nyingine siriasi.

Kinyume chake utapata umaarufu na mwisho wa siku utakuwa unabadili mapedeshee kwa kuwa watakupapatikia,” anasema Roseline John wa Kinondoni aliyewahi kufanya kazi hiyo miaka ya nyuma.

NINI CHA KUFANYA? Kama nilivyosema kuwa, wadada hawa wana umuhimu mkubwa kwenye tasnia ya muziki lakini siyo kazi ya kuitegemea tu.

Niwashauri tu ‘Mavideo Queen’ kama vile Kidoa, Gigy Money, Gilla, Kim Nana, Cute Bhinna, Tunda, Zuhura Gora, Baby Nahiyyah na wengineo kwamba kama mmejaaliwa muonekano mzuri na mkapata dili la kuonekana kwenye video za wasanii, fanyeni lakini tafuteni kazi nyingine halali za kuwaweka mjini.

Kumbuka wasanii watakutumia kwa kipindi f’lani lakini itafika wakati utakuwa huna dili tena, watatafutwa wasichana wengine, wewe utawekwa pembeni. Je, utafanya kazi gani? Akili kumkichwa binti!

Leave A Reply