Ma – Young na Ma – Dogo Mpaka Lini

Young D

1993 rapa mdogo machachari kutoka Unyamwezini, Shad Moss alipewa jina la Lil Bow Wow na mkongwe wa Hip Hop, Snoop Dogg. Licha ya kutamba na jina hilo kwa miaka kadhaa, 2002 aliamua kulibadilisha na kujiita Bow Wow kwa sababu aliyosema amekua mkubwa sasa na siyo Lil (Little) tena.

Hata hivyo, miaka 12 baadaye, rapa huyo aliyewahi kutamba na ngoma kibao ikiwemo Lets Get Down alibadili tena jina hilo, safari hii alijiita jina lake halisi alilopewa na wazazi wake, Shad Moss huku sababu ikiwa amekuwa baba wa familia na haoni umuhimu wa kutumia tena majina ya kisanii.

Mbali na Shad Moss kubadili jina, wapo wakali wengine kibao waliobamba wakiwa wadogo wakitumia majina ya kitoto na kuja kuyabadili. Miongoni mwa wakali hao ni Lil Romeo ambaye kwa sasa anajulikana kwa jina la Romeo.

Young Killer

Lakini pia mbali na Unyamwezini, Kibongobongo wapo wakali walioanzia kuwika wakiwa wadogo wakitumia majina ya kitoto, wakali hao ni Mr Blue ambaye wakati anaanza muziki akiwa na umri wa miaka 15 alipenda kujiita Lil Sam, Dogo Hamidu ambaye kwa sasa anaitwa Nyandu Tozi, Dogo Aslay sasa anatambulika kama Aslay na wengine wengi.

Licha ya baadhi ya wakali hao kuyabadili majina yao, wapo wengine kwao kubadili majina ya kitoto imekuwa tofauti, tangu walipotambulika na majina yao ya utoto hadi sasa wamekuwa wagumu kuyabadili.

Dogo Janja.

Wakali hao ni Young D aliyeanzia kukubalika kwenye Ngoma ya Tunapeta, Young Killer aliyeanzia kutambulika kwenye Ngoma ya Dear Gambe na Dogo Janja, ni ukweli uliowazi wakali hawa walianza muziki wakiwa machalii na walikuwa na kila sababu ya kujiita ‘Young’ Lil, Dogo na kadhalika.

Lakini kwa sasa wamekuwa wakubwa, ajabu makamanda hawa bado wanajiita majina yanayo wanathibitisha kwamba bado ni machalii. Kwao inawezekana kuona ni kawaida kujiita Ma-young na madogo lakini miaka inakwenda na wanazidi kujizolea mashabiki ndani na nje ya nchi.

Lakini kwa upande mwingine wanaweza kulifikiria hili la kubadili majina, kama wataona kuna maana watalichukua kama hawatajali basi wataliacha na kuendelea kuitwa madogo hadi watakapoacha muziki wakiwa wamezeeka


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment