The House of Favourite Newspapers

Maadhimisho ya Mwaka Mmoja wa Mzimu wa Afrika Zaidi ya Nchi 10 Zakutana Hapa Nchini

0

Dk. Riziki Mkali Malela akizungumza na wanahabari.                                                                                                                      Dar es Salaam 4 Septemba 2024: Wadau wa Tiba asilia kutoka katika nchi mbalimbali za Afrika wamewasili hapa nchini kwa ajili ya maadhimisho ya mwaka mmoja wa mzimu wa Afrika yanatarajiwa kufanyika hapo kesho Septemba, 5 hadi 7 katika Kijiji cha Kwa Msanja, Wilaya ya Chalinze, Mkoa wa Pwani.

Mtaalamu wa tiba asilia, Njilu Wambua kutoka Kenya akizungumza na wanahabari. (Hawapo pichani).

Maadhimisho hayo yamepewa umuhimu mkubwa na yatashuhudiwa matukio makuu yenye lengo la kuimarisha na kukuza tiba za asili katika eneo la Afrika na kubadilishana uzoefu kutoka kwa watumiaji wa tiba asilia kutoka nchi ya Tanzania, Kenya, Uganda, Congo, Malawi na nyinginezo.

Akizungumza na wanahabari leo, Dk. Riziki Mkali Malela, aliyekuwa mstari wa mbele katika maandalizi ya tukio hili, amesema maadhimisho haya yanalenga kuwatambulisha na kuwaunganisha watumiaji wa tiba asilia pamoja na wadau kutoka ndani na nje ya Bara la Afrika.

Dk. Riziki amesema maadhimisho haya yana umuhimu wa pekee katika kuwatambulisha wataalamu wa tiba asilia kutoka Afrika juu ya uwepo wa mzimu huo, pamoja na kushirikiana na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya Afrika. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA NEEMA ADRIAN 

Leave A Reply