The House of Favourite Newspapers

Maajabu ya binti aliyejifungua bila kujua ana ujauzito!

 

 

MSICHANA mwenye umri wa miaka 18, ambaye alizirai kwa muda wa siku nne baada ya kuumwa kichwa ameshangazaa kujikuta amejifungua mtoto wa kike.

 

Ebony Stevenson, mkazi wa Oldham, Uingereza, hakuwa anajua kama ana ujauzito na alienda kulala kwa sababu alikuwa hajisikii vizuri.

 

Msichana huyo alipelekwa hospitali baada ya kuonekana amepitiwa usingizi kwa muda mrefu, hivyo ndugu waliamua kumpeleka kupata huduma ya afya na kubainika kuwa ana ujauzito.

 

Mtoto wake alikuwa amejificha katika mfuko wa uzazi ambao nao ulikuwa umejificha, jambo ambalo huwa linatokea mara chache.

 

Kati miji miwili ya uzazi, mmoja ulikuwa unaendelea kumfanya dada huyo kuendelea kutoa hedhi huku mji mwingine ukiwa unakuza mtoto.

 

Mji huo wa mimba ulikuwa umekaa katika eneo la mgongo, jambo ambalo lilisababisha ujauzito usionekane.  Msichana huyo ambaye ni mwanafunzi wa michezo na yoga hakuwa amepata muonekano wa mimba, kuugua muda wa asubuhi au kukosa hedhi yake.

 

Msichana huyo ambaye amejifungua kwa mara ya kwanza, amesema kila kilichotokea kwake kupata mtoto kinamshangaza.

 

“Nina hofu namna nitakavyoweza kumlea mtoto wangu maana sikumuona hata wakati anatoka tumboni kwangu au kuhisi kuwa alikuwa tumboni kwangu, ila nafikiri kuwa ni mtoto mzuri sana.

 

” Huu ni muujiza mkubwa sana kwangu,” Ebony alieleza.

Ebony alifanyiwa upasuaji wa dharura ili ajifungue mtoto huyo, saa tatu baada ya kushtuka kwa nguvu kutoka kwenye usingizi mzito.

 

Mama yake binti huyo, Stevenson, mwenye umri wa miaka 39, alisema kuwa alipiga simu ya dharura baada ya mtoto wake kuanza kuumwa na kuanguka bafuni.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.